Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari za Kichunguzi, Erick Kabendera imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Septemba 12, 2019

Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na Mawakili wa Jamhuri kudai upelelezi wa kesi hiyo yenye makosa ya Uhujumu Uchumi, Utakatishaji fedha na Kukwepa kodi, bado haujakamilika.

Aidha, Wakili wa Utetezi, Jebra Kambole ameieleza Mahakama kuwa afya ya Kabendera imezorota baada ya kupata shida ya upumuaji hasa inapofika usiku.

Wakili Kambole ameeleza kuwa hali hiyo pamoja na miguu kukosa nguvu ilianza tangu Agosti 21 akiwa mahabusu.

Lugola atoa angalizo, 'Serikali haiwezi kuchezewa na Wanasiasa'
RC Chalamila awatangazia vita walioshambulia msafara wa DC Kitta