Kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, inaendelea lakini inaweza kuwa imejenga misingi ya utoaji wa haki kwa vyombo vya Serikali, mawakili na mahakama.
Lema alipata dhamana baada ya kukaa mahabusu kwa siku 121 kutokana na sarakasi za kisheria baada ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kuweka pingamizi dhidi ya dhamana yake alipofikishwa kortini kwa mara ya kwanza.
Akitoa dhamana hiyo, Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kaskazini amesema kuwa uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha kumpa dhamana Lema, Novemba 11 mwaka jana ulikuwa sahihi na hapakuwa na sababu za kupinga.
Aidha, akirejea kitendo cha Hakimu Mkazi wa Arusha kuacha kuendelea na masharti ya dhamana aliyompa Lema baada ya mawakili wa Serikali kumtaarifu kwa mdomo kuwa wana nia ya kukata rufaa kupinga dhamana hiyo.
Hata hivyo, Tangu wakati huo dhamana ya Lema ilikuwa ikikumbwa na migogoro ya kisheria iliyotinga hadi Mahakama ya Rufaa ambayo katika uamuzi wake iliweka bayana kuwepo kwa sintofahamu hiyo.

Magazeti ya Tanzania leo Machi 6, 2017
Rais Magufuli aiagiza Tanesco kukata umeme kwa Wizara zenye madeni