Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam,  imetoa maamuzi juu ya kesi ya maombi ya kupinga kuvuliwa ubunge iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, kwa maelezo kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Maamuzi hayo yametolewa leo Septemba 9, 2019 na Jaji Sirillius Matupa akieleza kuwa kesi hiyo ni ya Kikatiba hivyo inapaswa kufunguliwa kwa mfumo wa kesi ya uchaguzi na si kwa mfumo ambao alikuwa ameutumia mlalamikaji.

Jaji Matupa alifafanua kuwa  Mahakama hiyo haina mamlaka ya kutengua ubunge wa Miraji Mtaturu, aliyeapishwa hivi karibuni kuwa mbunge wa Singida Mashariki.

Kesi hiyo namba 18 ya mwaka 2019, Lissu aliiomba Mahakama impe kibali cha kufungua shauri la kupinga taarifa ya Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kufuta ubunge wake, ambapo Mahakama imetupilia mbali shauri hilo.

Kwa upande waupande wa mawakili wa Lissu, wameahidi kwamba watajipanga upya ili  kufungua kesi ya uchaguzi kama ilivyoelekezwa na Mahakama hiyo.

Kutokana na uamuzi huo wa Mahakama, Julius Mtaturu (CCM) ataendelea kuwa Mbunge wa Singida Mashariki.

Kijana wa miaka 17 apata upofu wa macho kwa kula chips
Juma Kaseja alamba Milioni kumi, Makonda amkabidhi