Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kusikiliza kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa sababu ya matatizo ya kiafya.
Hayo yameelezwa leo mbele ya hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri baada ya wakili wa serikali, coustantine Kakula kueleza shauri hilo limesitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.
Hata hivyo, wakili wa Masogange, Ruben Simwanza alimueleza Hakimu kwamba mteja wake anaumwa hivyo anaomba kesi ihairishwe.
Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 25, 2017 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.
Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili yaliyosomwa na mwendesha mashtaka Mashauri Wilboard chini ya wakili wa serikali Constatine , akidaiwa kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepan kwa nyakati tofauti.
Kupitia mashtaka hayo, Masogange aliachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.
Hata Hivyo hii sio mara ya kwanza kwa Masogange kushikiliwa na polisi kwa tuhuma hizo. August 2014, Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kilimhoji kwa zaidi ya saa 10 mrembo huyo kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka 2014.