Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu imeahirishwa baada ya shahidi wa Jamhuri kushindwa kufika mahakamani kwa madai ya tatizo la kiafya.

Hata hivyo Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando, aliiomba Mahakama iahirishe kesi mpaka kesho kwa kuwa shahidi wao amepata tatizo la kiafya.

“Shauri linakuja kwa ajili ya kusikilizwa mpaka jana kuna shahidi ambaye tulikuwa tumepanga kuendelea naye lakini amepata tatizo la kiafya. Hivyo tunaomba ahirisho mpaka kesho tutakapoweza kuendelea. Suala hili liko nje ya uwezo wetu” Kidando.

Naye Wakili Peter Kibatala upande wa Utetezi wamekubali ombi hilo ambapo ameeleza kuwa “Kwa kufuata amri ya Mahakama ya jana sisi tulikuwa tumejiandaa lakini kwa kuwa mambo yako hivi hatuna namna ila tunaomba tu wenzetu wajitahidi kesho tarehe 4 tuweze kuendelea.” wakili Peter Kibatala.

Jaji Joachim Tiganga ameahirisha kesi hiyo hadi Kesho Alhamisi Novemba 4, 2021.

“Upande wa mashtaka mnakumbushwa kuanda mashahidi ili tuweze kuendelea. Washtakiwa mtaendelea kuwa chini ya uangalizi wa Magereza” Amesema Jaji Tiganga.

CAF yaichinja Biashara United Mara
Mkuu wa Uhamiaji: Wahamiaji haramu 1,152 wamekamatwa Kagera