Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan afanye analoweza kushughulikia kesi ya Mbowe na wenzake watatu, baada ya kukutana naye mjini Brussels.
Amesema kesi ya Mbowe na wenzake ni Moja ya ajenda iliyokuwepo kwenye ujumbe wa CHADEMA kwa Rais Samia, wenye ajenda mbalimbali
Akizungumza kwa njia ya mtandao baada ya kukutana na Rais na kufanya naye mazungumzo ya takriban saa moja Lissu amesema Rais Samia amemuahidi kushughulikia kesi hiyo.
Lissu amesema kuwa kesi hiyo ya Mbowe na wenzake haisaidiii Tanzania , haisaidiii chama ch a CHADEMA lakini pia haisaidiii Chama Cha Mapinduzi CCM.