Hukumu ya kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe dhidi ya mwanahabari Cyprian Musiba imeahirishwa hadi Oktoba 28, 2021.
Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe anamdai Musiba fidia ya jumla ya Sh10.3 bilioni kwa madai ya kumkashfu, kupitia magazeti yake ya Tanzanite.
Wakili wa Membe, Jonathan Mndeme amesema hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa itolewe leo Jumanne Oktoba 12, 2021 na Jaji Joaquine De Mello imeahirishwa kwa sababu haijakamilika kuandikwa.
Mbali na Musiba, wadaiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa Gazeti la Tanzanite linalomilikiwa na Musiba, na kampuni ya Tz Information and Media Consultant Ltd.
Mwanahabari Cyprian Musiba ambae amkua akijiita mwanaharakati huru amekua mstari wa mbele kuandika habari zinazohusiana na viongozi na watendaji wa serikali hasa inapotokea mkanganyiko katika utendaji na utoaji wa taarifa.