Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu ambaye amefungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kujihusisha na filamu kwa muda usiojulikana kwa kosa la kusambaza picha zenye maudhui ya kingono leo amefikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.
Wema ambaye alifunguliwa kesi hiyo na Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) ameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 10.
Amesomewa shtaka hilo na wakili wa Jamhuri, Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakim Mkazi, Maila Kasonde katika mahakama ya Kisutu.
Wema anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 15, 2018 la kuchapisha video yenye maudhui ya ngono na kurusha katika mtandao wake wa kijamii wa Istagram.
Wema ametakiwa kusaini bondi ya milioni 10 pamoja na mdhamini wake mmoja na ameachiwa huru huku akitakiwa kurudi tena mahakamani Novemba 11, 2018 kusikiliza kesi yake.