Kiungo wa Vinara wa Ligi Kuu ya England Manchester City, Kevin de Bruyne amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo  ambayo inaendelea kuwa tishio ndani nan je ya England.

De Bruyne ambaye alijiunga na Manchester City mwaka 2015 akitokea VfL Wolfsburg ya Ujerumani, amesaini mkataba mpya ambao utafikia kikomo mwaka 2025.

Mkataba wa awali wa De Bruyne mwenye umri wa miaka 29 ulikua unafikia kikomo mwaka 2023.

Mpaa sasa kiungo huyo kutoka nchini Ubelgiji ameshinda mataji mawili ya Ligi ya England (EPL), Kombe la FA na Kombe la Ligi (Carabao Cup) mara nne tangu ajiunge na The Citizens.

De Bruyne amekuwa muhimu sana kwa kikosi cha Pep Guardiola msimu huu ambao wanakaribia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya England, licha ya Msimu wake kuingiliwa na majeraha, De Bruyne amefunga mabao manane na kutoa Assists 16 katika mechi 33.

Alifunga bao la ufunguzi katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa jana Jumanne (April 06) dhidi ya Borussia Dortmund na alishiriki kutengeneza bao la ushindi dakika za lala salama likifungwa na Phil Foden.

Mayay: Hawa jamaa ni hatari kwa sasa
Simba SC yawasili Cairo, Misri