Klabu ya AS Roma ya nchini Italia imeafiki kumuuza kiungo kutoka Uholanzi Kevin Strootman, baada ya kufanya biashara na Olympique de Marseille ya Ufaransa.
Usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, umeigharimu klabu ya Olympique de Marseille inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa kiasi cha Euro milioni 25 sawa na dola za kimarekani milioni 28.6.
Strootman ambaye tayari ameshaitumikia timu ya taifa ya Uholanzi katika michezo 41, anaondoka AS Roma baada ya kuichezea klabu hiyo kwa muda wa miaka mitano, akisajiliwa kutoka PSV Eindhoven.
Msimu uliopita kiungo huyo aliitumikia AS Roma katika michezo 32 ya ligi, na kufunga bao moja.
Marseille ambao kwa sasa wanashika nafasi ya tisa kwenye msiammo wa ligi ya Ufaransa, huenda wakamtumia kiungo huyo katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili utakaowakutanisha na AS Monaco.