Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameagiza Makandarasi au Mameneja wanaolazimisha wananchi kulipia nguzo za umeme ili kuunganishiwa nishati hiyo kukamatwa.
Amesema watu hao wanapuuza agizo la Serikali linalotaka nguzo hizo kutolewa bure baada ya kupokea malalamiko ya Mwenyekiti wa CCM, Simiyu, Enock Yakobo.
Yakobo amesema licha ya Serikali kutangaza mara kwa mara kuwa nguzo za umeme ni bure wapo makandarasi wanaoendelea kukaidi agizo hilo na kuwatoza wananchi fedha.
Kalemani amewataka wakuu wa Wilaya kote nchini kusimamia agizo hilo na kuwakamata watakaotoza fedha kwa kuwa Serikali inatoa nguzo bure na wananchi wanapaswa kuchangia Tsh. 27,000 ili kuunganishiwa umeme.