Klabu ya Crystal Palace imemtimua Frank de Boer ambaye amedumu siku 77 tu katika kibarua chake akiwa kocha wa timu hiyo akiwa ameiongoza kwa michezo mitano pekee.

Crystal Palace wapo katika nafasi ya 19 ya msimamo wa ligi ya Uingereza baada ya kufungwa bao 1-0 na klabu ya Burnley siku ya Jumapili huku ikiwa haijafunga bao hata moja katika michezo yote minne ya ligi kuu.

Frank de Boer mwenye umri wa miaka 47 anakuwa kocha wa kwanza katika ligi ya Uingereza kufukuzwa ndani ya muda mfupi akiwa ameiongoza timu yake kwa michezo michache zaidi.

De Boer alichukua nafasi ya Sam Allardyce aliyeisaida Crystal Palace kuepuka kushuka daraja msimu uliopita katika ligi ya Uingereza.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Ajax alishinda ubigwa wa ligi kuu ya Uhoranzi mara nne mfurulizo akiwa na Ajax kabla ya kuhamia Inter Milan ambapo pia alitimuliwa mwezi Novemba mwaka 2016 baada ya kudumu katika kalbu hiyo kwa siku 85.

Mwenyekiti wa klabu ya Crystal Palace Steve Parish amesema klabu pamoja ma mashabiki hawajafurahishwa na hali ilivyo ndani ya timu yao kwa sasa na wanadhani hawastahili kuendelea hivyo.

”Nani ana kikosi kizuri, sisi au Burnley? tulimaliza katika nafasi ya 11 msimu uliopita tukiwa na kikosi dhaifu sijawahi kukataa hilo lakin mambo yanaenda vibaya kwa sasa” alisema Steve Parish.

De Boer alifanya usajili wa wachezaji wawili kwa kumsajili Mamadou Sakho kutoka Liverpool kwa pauni milioni 26 na Jairo Riedewald kutoka Ajax kwa pauni milioni 7.9.

 

 

LIVE: Kimbunga Irma chaitikisa Marekani
Gwajima mbioni kuwatumbua watu wasiojulikana