Uongozi wa klabu ya Leicester City, umetangaza kuachana na meneja Nigel Pearson, ambaye alikiongoza kikosi cha klabu hiyo kucheza ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu wa 2014-15.

Uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kumtimua kazi meneja huyo usiku wa kuamkia leo, huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Pearson mwenye umri wa miaka 51, alionyesha kupambana vilivyo katika ligi ya msimu uliopita na kuibakisha Leicester City katika michuano ya ligi kuu na kuiwezesha kumaliza katika nafasi ya 14.

Pearson alipewa jukumu la kuanza kazi ya kukiongoza kikosi cha The Foxes kuanzia mwezi November, 2011.

Blatter Ahofia Kwenda Kutazama Fainali za Wanawake kisa kashfa
Yanga Yakubali Kuwaachia Wachezaji Watatu