Everton ikicheza katika uwanja wake wa Goodison Park hapo jana ilipokea kipigo cha mabao 5-2 kutoka kwa Arsenal na kushuka mpaka nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ‘EPL’.
Wyne Rooney alitangulia kuipataia Everton bao la kuongoza dakika ya 12 lakini kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza Nacho Monreal aliifungia Arsenal bao la kusawazisha dakika ya 40.
Kipindi cha pili dakika ya 53 Mesut Ozil aliipatia Arsenal bao la pili na mambo yalionekana kuwa magumu zaidi kwa Everton hasa baada ya mchezaji Idrissa Gana Gueye kutolewa nje kwa kadi nyekundu hali iliyotoa mwanya kwa Arsenal kutawala mchezo na kufunga mabao mengine matatu kupitia Alexandre Lacazette, Aaron Ramsey na Alexis Sanchez.
-
Man Utd yaambulia kipigo huku Man City ikizidi kujikita kileleni EPL
-
Yanga yapeleka salamu kwa wekundu wa Msimbazi
-
Polisi waanza uchunguzi baada ya ugomvi wa wachezaji wa Everton na Lyon
Matokeo hayo yanamuweka kocha Ronald Koeman katika wakati mgumu kwani pamoja na uwekezaji ambao klabu ya Everton Imeufanya kwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kununua wachezaji wapya bado timu hiyo imeshindwa kupata matokeo ya kuridhisha na sasa ikiwa imeshuka mpaka nafasi ya 18.
Mwenyekiti wa Everton Bill Kenwright alitarajia timu yake itoe changamoto kubwa msimu huu na ndio maana haikuwa shida kwa Everton kutoa kiasi cha £140 kununua wachezaji ila kwa kinachoendelea hadi sasa ni wazi atakuwa ameanza kuchoka hali hii.
Si kwamba Everton imesajili wachezaji wabovu kwani kuwa na Rooney,Michael Keane, Sandro au Siggurdson huwezi kusema unawachezaji wabovu lakini tatizo la Everton ni umaliziaji tu kwani inaonekana wameshindwa kuziba pengo la Romelu Lukaku.