Watoto wawili wa familia moja kata ya kishanda katika Halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera wameteketea kwa moto wa kibatari wakiwa wamelala.

Moto huo unavyotokea wazazi wa watoto hao walikuwa kwenye biashara zao za kuuza duka.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi alisema watoto hao waliachwa wenyewe wakiwa wamelala na kibatari kikiwa kinawaka huku wazazi wao wakiwa katika biashara.

Aliwataja watoto walioteketea kwa moto kuwa ni Jaksoni Kebini mwenye umri wa miaka 4 na mdogo wake Deograta Kebini mwenye umri wa zaidi ya mwaka mmoja.

Kamanda alisema chanzo cha moto huo ni kibatari ambacho kiliachwa kinawaka ambapo kilianguka na moto kuanza kusambaa na kuanza kushika nyasi na kusambaa katika chumba walichokuwa wamelala watoto hao na kuteketea kwa moto.

Ametoa wito na tahadhari kwa wananchi kwamba wanapotoka wasiwaache watoto katika mazingira kama hayo kwani ni kuhatarisha usalama wao.

Wanachuo wavalishwa mabox kukomesha udanganyifu wa mtihani
Afariki dunia akidungwa sindano ya kuongeza makalio