Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema imebainika kuwa waliojihusisha na vitendo vya mauaji ya Watanzania 9 kwa kuwapiga risasi na wengine kushambuliwa kwa mapanga ambao ni watu wasiojulikana, walianza chokochoko hizo eneo la Kibiti mkoani Pwani na walipo vulumishwa na Jeshi la Polisi wengine walikimbilia nchi jirani ikiwemo Msumbiji.
Mauaji hayo yalitekelezwa na watu waliokuwa wamevaa sare za Jeshi kwenywe kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, pembezoni mwa mto Ruvuma.
IGP Sirro amesisitiza kuwa wauaji hao watasakwa popote walipo na watachukuliwa hatua za kisheria.
Ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizunguza na wakazi wa kata ya Kitaya halmashauri ya Wilaya ya Mtwara alipofanya mkutano wa hadhara mara baada ya kutembelea kata hiyo kwa lengo la kuwasalimia na kuwapa pole waathirika wa mauaji hayo.
Juni 26 mwka huu wanawake watatu na mtoto mmoja walishikiliwa na pia wanawake saba walitekwa kwa muda wakati wa tukio hilo la mauaji likitokea na kisha wakaachiwa, huku mmoja katiyao alitumwa ujumbe aulete kwa serikali ya Tanzania.
Mkuu huyo wa Polisi ametuma salamu kwa wahusika wa mauaji hayo kuwa Tanzania ni nchi yenye amani ila kwa wale ambao hawajazoea amani watapata tabu.
Mtanzania Fatuma Masudi aliyenusurika katika mauaji hayo alipewa ujumbe aufikishe Tanzania ulioandikwa “Tunakupa salamu uende ukaseme huko kwenu yakikauka tu maji tunavuka sisi wala hatuogopi nenda kaseme”
Hata hivyo Serikali ya Tanzania leo inakutana na Serikali ya Msumbiji ili kuweka mambo sawa kufuatia tukio hilo, huku watanzania wakitahadharishwa kutoenda nchini humo kwa sasa hadi hapo hali itakavyokuwa shwari.