Nassor Binslum ni mmoja wa wafanyabiashara na matajiri wanaopenda michezo nchini. Binslum ndiye mdhamini wa Mbeya City ambayo nahodha wake Juma Nyoso amekumbwa na kashfa ya udhalilishaji dhidi ya John Bocco wa Azam ametoa tamko.

Taarifa yake rasmi ni kama ifuatavyo; “Nimekua nikiulizwa maswali mengi juu ya sakata la Juma Nyosso kutoka kwa marafiki, wateja wangu na wadau wa soka kwa ujumla mbona tukiwa kama wadhamini wa Mbeya City kupitia moja ya bidhaa zetu Rb Battery tumekua kimya na hatujatoa tamko lolote mpaka sasa.”

“Tamko langu kwa niaba ya kampuni yetu ya Binslum Tyres Co Ltd ni hili hapa; Tunalaani tukio hilo kwa nguvu zetu zote kwa nahodha wa timu ambaye ndiye muwakilishi mkuu wa klabu, wadhamini pamoja na wananchi wa Mbeya kwa ujumla kwa tukio hilo alilomfanyia nahodha mwenzake wa Azam Fc John Bocco.

“Ni tukio linalochukiza na si tu kuuchafua mchezo wa soka bali pia kutuchafua sisi wadhamini na washirika wenzetu pamoja na wananchi wa mkoa wa Mbeya, binafsi na kwa niaba ya kampuni yetu tunaunga mkono adhabu kali aliyopewa Nyoso, mwisho ningependa kumalizia kuwaomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na hata waandishi wa habari wafanye weledi huu wa kuripoti unyama wa aina hii.

“Sambamba na adhabu kali kwa Klabu na Wachezaji wote nchini wenye tabia hizi chafu kwani siamini kama Nyoso hizi tabia ameanza leo au jana bali ni tabia alizotokanazo kote alipopitia lakini hakuwahi kuadhibiwa huko nyuma wala kuripotiwa katika magazeti mpaka sasa amekua mchezaji wa Mbeya City na pia siamini mwenye tabia hizi chafu ni Nyoso peke yake bali wako wengi katika wachezaji wetu tena wengine wakichezea klabu kubwa zenye mashabiki wengi nchini lakini hatujaona hata siku moja weledi huu uliotumika kumtia Nyosso hatiani ukitumika katika usawa uleule kwa matukio ya aina ileile.” Mwisho wa taarifa ya Binslum.

Rodgers Apewa Nafasi Nyingine Ligi Ya England
Wenger Awachimba Mkwara Wachezaji Wake