Timu ya Taifa “Taifa Stars” leo Jumapili (Mei 29) imeanza mazoezi rasmi ya kujandaa na michezo ya kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Niger na Algeria itakayochezwa mapema mwezi ujao.

Stars imeanza mazoezi yake Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku asilimia kubwa ya wachezaji wa Simba SC ana Young Africans wakiwa sehemu ya mazoezi hayo.

Wachezaji wa klabu hizo kongwe walilazimika kurejea haraka jijini Dar es salaam, baada ya timu zao kumenyana jana Jumamosi (Mei 28) jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba, na Simba SC kuambulia kichapo cha 1-0.

Kibu Denis na Kibwana Shomari ambao walizua hofu katika mchezo huo baada ya kugongana wakiwa kwenye harakati za kuwania mpira, wameonekana kwenye mazoezi hayo, hali ambayo imethibitisha wapo sawa kiafya.

Nahodha na Mshambuliaji wa Stars Mbwana Samatta anayecheza soka nchini Ubelgiji na Simon Msuva nao wameonekana katika mazoezi ya leo.

Stars itaanzia ugenini Niger Juni 4, 2022 kisha itarejea nyumbani kucheza dhidi ya Algeria Juni 8, 2022, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Azam FC chalii, Coastal Union yaifuata Young Africans
Nachingwea kujenga kituo kukabiliana na Tembo