Baada ya kushuhudia timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20 ‘The Tanzanite’ ikichapwa mabao 6-0 dhidi ya Nigeria katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia, Waziri

mwenye dhamana ya michezo Dr Harrison Mwakyembe ametoa neno kwa kusema  sasa serikali itaweka nguvu kwenye soka la wanawake.

Kutona na matokeo hayo yaliyofatikana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Tanzanite imeondolewa kwenye mchakato huo kwa jumla ya mabao 9-0 baada ya kupoteza pia mchezo wa awali kwa magoli 3-0 huko nchini Nigeria.

Akizungumza zaidi, Waziri Mwakyembe alisema: “Wadau wa michezo wamemaliza kuijadili sera ya michezo, nitaletewa taarifa baada ya siku chache zijazo. Ninauhakika hilo suala limegusiwa kwa nguvu sana kwa sababu hili taifa letu tuna maeneo ambayo mtoto wa kike kucheza mpira anaonekana si mtoto wa kike na kuna wazazi wako tayari kumfukuza mtoto nyumbani.”

“Kuna suala la kubadili fikra kwa wazazi lakini na sisi kama Wizara na TFF tuna kazi kubwa kuhakikisha tunaweka nguvu zaidi kwenye soka la wanawake, ni muhimu sana kufanya hivyo.”

“Kuna wazo la kuanza Taifa Cup kwa ajili ya wanawake tu ili ndani ya miaka mitatu au miwili ijayo tuwe na timu imara ya wanawake.”

Haji Manara atupa kombora nyumba ya jirani
Watu 50 wauawa kwa risasi kwenye tamasha Marekani