Kiungo mshambuliaji Shizza Ramadhan Kichuya amesema hajajiunga na Namungo FC mkopo, kama inavyoendelea kuelezwa katika vyanzo mbalimbali vya habari, bali ametua kwa wawakilishi wao wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika akiwa kama mchezaji huru.
Kichuya ambaye alionekana mwishoni mwa juma lililopita akiwana Namungo FC wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam FC, amesema amesajiliwa na klabu hiyo baada ya mkataba wake miezi sita na Simba SC kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2019/20.
Hata hivyo Kichuya ameshindwa kuweka wazi mkataba wake na Namungo FC huku akisisitiza wanaofahamu kama yupo klabuni hapo kwa mkppo wanapotoshwa.
”Nilipomaliza mkabata wangu wa miezi sita na Simba, nilifuatwa na timu nyingi lakini mimi na meneja wangu tukaona sehemu ya kwenda na kurudisha ubora wangu ni Namungo FC, ninaamini kupitia hii timu nitafanya vizuri hata kuliko Simba.” Amesema Kichuya.
Mshambuliaji huyo ameongoza kusema licha ya mkataba wake kumalizika ndani ya Simba lakini ukosefu wa namba ulichangia kuondoka kwa mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho 2019.
Akiwa Simba SC msimu wa 2019/20 alifunga bao moja kati ya mabao 78 yaliyofungwa na timu hiyo ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao moja kwa moja dhidi ya Ruvu Shooting.
Kikosi cha Namungo FC kinaratajiwa kuondoka Dar es salaam kesho kuelekea jijini Arusha, tayari kwa mchezo wa Ngao Jamii dhidi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC utaopigwa siku ya jumapili Agosti 30.