Wanafunzi 490,103 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne, ambao umeanza leo Novemba 23 ikiwa ni ongezeko la 0.9% la waliofanya mitihani hiyo 2019, wavulana wakiwa ni 213,553 (47%) wasichana ni 234,103 (52.3%)

Akizungumza Ofisini kwake Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Sekondari, Benjamin Oganga amesema, wanafunzi hao wanaanza rasmi mitihani hiyo kuanzia leo Novemba 23 hadi Disemba 11, 2020.

Oganga, amefafanua kuwa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu kutoka kundi la watahiniwa binafsi ni 11, saba wakiwa ni wenye uoni hafifu na 4 wasioona.

Mwaka 2019 jumla ya Wanafunzi waliofanya mtihani wa kuhitmu kidato cha Nne walikuwa 485,866, mwaka huu kukiwa na ongezeko la wanafunzi 4,237 sawa na asilimia 0.9.

Mkurugenzi huyo amehitimisha kwa kuwatakia kila la kheri wanafunzi wote walioanza mitihani hiyo leo.

Mkwasa akataa ubingwa VPL
Kagere, Miquissone watinga kambini Arusha