Wanafunzi wa kidato cha sita na kozi za ualimu wanatarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu hapo kesho Jumatatu Mei 7, 2018.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la mitihani (NECTA), Charles Msonde alipokuwa anaongea na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam.

Ambapo jumla ya shule za sekondari 674, Vyuo vya ualimu 125 na vituo vya kujitegemea 231 vimesajiliwa kufanya mitihani hiyo Tanzania Bara na Zanzibar.

Msonde amesema kwa mwaka huu wapo watahiniwa 12 wasioona kabisa na watahiniwa wenye uono hafifu 56 ambapo maandishi ya karatasi zao hukuzwa ili kuwasaidia kuona vizuri, amasema kuwa jumla ya watahaniwa 77,643 wamesajiliwa kufanya mitihani ya kidato cha sita ambapo watahiniwa 77,222 wanatoka katika shule za sekondari na watahiniwa 10,421 ni watahiniwa wa kujitegemea huku watahiniwa 7,462 wamesajiliwa kufanya mitihani ya kozi za ualimu ngazi ya cheti na stashahada.

Aidha Baraza la Mitihani la Taifa limetoa wito kwa kamati za mitihani za Mikoa, Halmashauri, Manispaa na Majiji kuzingatia taratibu zote za uendeshaji wa mitihani ya taifa, Baraza hilo pia limewataka wasimamizi wote wa mitihani kufanya kazi yao kwa umakini na uhadilifu huku wakijiepusha na vitendo vya udanganyifu.

Uongozi wa Dar24 Media unawatakia mitihani mema watahiniwa wote watakaofanya mitihani yao ya kuhitimu kuanzia kesho.

 

Madaktari watoa ripoti upasuaji wa Ferguson, ''anahitaji kupumzika''
Mhagama aweka jiwe la msingi jengo la kutoa huduma za matunzo Tiba (CTC)