Mwanamuziki kutoka Burundi Niyimbona Jean Pierre maarufu kwa jina la Kidumu amelazwa kwenye hospitali moja nchini humo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikula sumu.
Kidumu ambaye makazi yake ni nchini Kenya ameweka wazi swala hilo kupitia mitandao yake ya kijamii, ambapo amedai amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu asiowafahamu hivyo anahusisha tukio hilo na vitisho hivyo.
Aidha, Muimbaji huyo ambaye alikuwa njiani kurudi nchini Kenya ambako ndiko yalipo makazi yake amesema hali yake bado ni mbaya kutokana na sumu kuendelea kuwepo mwilini mwake.
‘Ilikuwa niruhusiwe lakini hospitali imebadilisha maamuzi kwasababu wamegundua sumu imeingia kwenye figo, mniombee, maadui zangu wanatakiwa kushindwa kutokana na sara zenu’’ ameandika Kidumu kwenye mtandao wa kijamiii.
-
China yathibitisha ziara ya Kim Jong Un, ajipanga kumuona Trump
-
Mahakama nchini Kenya yamkingia kifua Miguna
Mkali huyo wa wimbo wa Number Moja, Ambaye kwasasa anafanya muziki wa injiri hivi karibuni amekuwa akijihusisha katika kuwaunganisha wananchi wa Burundi kufuatia kuwepo kwa taharuki za kisiasa zikihusisha serikali inayoongozwa na raisi Piere Nkurunziza.