Kifo cha Ndugu wa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Nam, aliyefariki dunia katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur nchini Malaysia, kimegubikwa utata, huku chanzo cha kifo hicho kikizua sintofahamu nchini humo.
Polisi nchini Malaysia wamesema kuwa Kim Jong Nam alishambuliwa siku ya Jumatatu wakati alipokuwa akitarajia kusafiri kuelekea Macao, Kabla hajafariki dunia wakati akipelekwa hospitalini, alitoa maelezo kuwa alivutwa kutoka kwa nyuma na kumwagiwa kimiminika usoni mwake.
Aidha, Uchunguzi unatarajiwa kufanywa na jopo la madaktari ili kuweza kubaini chanzo cha kifo chake, huku kukiwa na tetesi kuwa huenda kimiminika alichomwagiwa usoni huenda ikawa ni simu.
Hata hivyo, chanzo kutoka katika Serikali ya Marekani kimesema kwamba wanaamini kwa dhati kuwa Kim, aliyekuwa anaishi uhamishoni ameuawa na majasusi kutoka Korea Kaskazini.