Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Watumishi watatu wa kituo cha Afya Kabuku kilichopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na uzembe uliosabaisha kifo cha mama mjamzito na kichanga chake.
Waziri Ummy amesema tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba ametua timu kutoka katika ofisi ya mganga mkuu wa mkoa inayojumuisha madaktari bigwa wawili, daktari bingwa wa wanawake na uzazi na daktari bingwa wa huduma za usingizi ili kufanya uchunguzi wa tukio hilo
”Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Handemi amewasimamisha kazi watumishi watatu walioshiriki kumpatia huduma mama huyo tangu alipopokelewa kituoni hadi umauti ulipomkuta ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo baya na lisilopaswa kuvumiliwa,” amesema Ummy.
Aidha, amesema kuwa tuhuma hizi tayari zimeshapokelewa na mabaraza ya kitaaluma (MCT), (TNMC) na vyombo vingine vya dola kwaajili ya uchunguzi zaidi hivyo ninaelekeza mabaraza haya ndani ya siku 7 kuanzia leo kuniletea taarifa ya uchunguzi wa tukio hili na mapendekezo ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
”Ni wahakikishie umma wa watanzania kuwa umma wa watanzania kuwa baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi kila mtumishi aliyehusika atachukuliwa hatua za kitaaluma, kiutumishi na kjinai ikiwemo kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kijinai pale itakapothibitika”