Aliekuwa Mtendaji  Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) Laurian Bwanakunu na mwenzake, wanaoshtakiwa kwa uhujumu uchumi wanaendelea kusota rumande, kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki ambao kesi yao iko mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mmbando.

kesi hiyo yenye mashtaka matano yakiwemo kuisababishia Serikali hasara Shilingi bilioni tatu ilipokuwa ikitajwa na kuahirishwa hadi Oktoba 5 mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, inadaiwa walitenda kosa hilo kati ya Julai Mosi mwaka 2016 hadi Juni 30 mwaka 2019, washitakiwa hao wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao kwa kuendesha genge la uhalifu kwa kujipatia faida.

Inadaiwa, katika tarehe hizo wakiwa ofisi za MSD zilizopo Keko, Wilaya ya Temeke Dar es Salaam, washtakiwa hao kwa vitendo yao viovu waliisababishia MSD hasara ya Sh 3, 816,727,112.75  (karibu Sh bilioni 3.8).

Katika shtaka jingine, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Bwanakunu katika tarehe hizo, akiwa mtumishi wa umma alitumia vibaya madaraka yake kwa kukiuka sheria ya utumishi wa umma kwa kuwalipa wafanyakazi wa MSD Sh 3,816,727,112.75 kama nyongeza ya mshahara na posho ya pango la nyumba, bila kibali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Utumishi wa umma.

Pia katika shtaka jingine, washtàkiwa hao kwa pamoja, wanadaiwa kuwa katika tarehe hizo, kwa uzembe wa kutohifadhi vyema vifaa tiba na dawa na kufanya viharibike visitumike na hivyo kuisababishia MSD hasara ya Sh 85, 199, 879.65.

Washtakiwa hao pia wanakabiliwa na shitaka la utakatishaji fedha kwamba,  katika tarehe hizo, wote kwa pamoja walijipatia Sh 1,603,991,095.37 wakati wakijua fedha hizo zimetokana na kosa la kushiriki genge la uhalifu.

Kenya: Jaji mkuu amtaka rais kulivunja Bunge
Gwajima, Pengo, Makonda Uso kwa Uso