Jeshi la polisi mkoani Kigoma limewakamata watuhumiwa 146 kupitia operasheni maalum kutokana na matukio matatu yaliyofanyika kati ya Agosti 25 na 30 mwaka huu.

Mkuu wa Oparesheni Maalum, Mihayo K Msikhela amesema kati ya watuhumiwa waliokamatwa, 141 ni wahamiaji kutoka nje ya nchi na watano ni wenyenyeji ambao wanatumika kuwahifadhi waharifu hao.

Mihayo ameyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na mauaji lililofanyika Agosti 25, baada ya gari aina ya Toyota Hiace kutekwa na watu saba waliompiga na risasi kichwani dereva wa gari hilo, Maisha Musa almaarufu kama Kabudo na kusababisha kifo chake.

Amesema majambazi hao walipora kiasi cha fedha zaidi ya Milioni 2 na simu nane.

Tukio lingine ni washukiwa watano wakiwa na bunduki moja na silaha za jadi walivamia nyumba ya mkulima Yuda Yohana na mkazi wa Nanchenda wilaya kasulu na kumpora kiasi cha shilingi elfu kumi na simu mbili za techno na kutokomea kusikojulikana.

Na tukio la tatu ni unyang’anyi wa kutumia nguvu katika maeneo ya Kamve, kijiji cha Kumtundu, Wilaya ya Kasulu kwenye barabara kuu itokayo Kibondo kwenda Kasulu.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi, mfanyabiashara Juma Samayombe akiwa na mwenzake kwenye gari binafsi waliporwa fedha taslimu zaidi shilingi milioni moja na simu tatu baada ya kukuta magogo barabara.

Mkuu huyo wa opareshi maalum amesema watu wenye nia mbovu wanaotoka nchi jirani wataingia lakini hawatatoka salama.

“Tutahakikisha tunawakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria,” amesema.

KMC FC: Tupo tayari kwa Ligi Kuu 2020/21
Griezmann ahakikishiwa nafasi FC Barcelona