Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango jana aliwasilisha  bungeni mjini Dodoma Bajeti Kuu ya Serikali ya Awamu ya Tano na kuainisha mikoa mitano yenye umasikini zaidi nchini.

Dk Mpango

Dk. Mpango aliutaja mkoa wa Kigoma kuwa ndio mkoa unaoongoza zaidi kwa kuwa na wananchi wanaoishi katika umasikini wa kipato uliokithiri. Alisema asilimia 48.9 ya wananchi wa Mkoa huo wanaishi katika kiwango hicho cha umasikini.

Mikoa mingine minne iliyotajwa katika mstari wa umasikini uliokithiri nchini na asilimia ya wananchi wanaoishi katika kiwango hicho kwenye mabadoni ni Geita (43%), Kagera 39%, Singida 38.2% na Mwanza 35.3%.

Katika hatua nyingine, Dk. Mpango aliitaja mikoa ambayo ina unafuu katika kiwango cha umasikini wa kipato nchini kuwa ni Dar es Salaam (5.2%), Kilimanjaro (14.3%), Arusha (14.7), Pwani (14.7) na Manyara (18.3).

Bajeti iliyowasilishwa yenye shilingi trilioni 29.5, kati ya hizo shilingi trilioni 11.82 ni kwa ajili ya Maendeleo. Bajeti hiyo inatarajiwa kuwa chanzo cha kupunguza umasikini na utegemezi nchini.

 

Video: Posho Yawapitia Mbali Wabunge Waliotoka Nje ya Ukumbi wa Bunge
Video: Magazeti Leo 09-Jun-2016