Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewapa pole wana simba wenzake huku akihoji mishahara ya Sh bilioni 4 aliyolipa mwekezaji wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji (Mo) amelipa kwa makubaliano gani.
Kigwangalla alihoji swali hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akisema isije kuwa fedha hizo ni ile bilioni 20 ya manunuzi ya hisa ya asilimia 50.
“Ama manunuzi yalikwishafanyika? Anavyojitoa italipwaje? # NguvuMoja,”. Aliandika Kigwangalla.
Dk. Kigwangalla aliandika ujumbe huu katika ukurasa wake wa Twitter.
” Poleni wanasimba wenzangu ‘ kisukari kimetuvuruga hivi kuna mtu anaweza kunisaidia? Hii mishahara ya 4bn iliyolipwa na Mo inalipwa kwa makubaliano gani? Isije kuwa ndiyo katika ile 20 bn ya manunuzi ya hisa 50% ama manunuzi yalikwishafanyika? Anavyojitoa, italipwaje? # NguvuMoja,”.
Jana Mo alitangaza kujiudhuru nafasi yake ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba.
Alisema ni jambo la huzuni kwa klabu ya @SimbaSCTanzania kutoshinda licha ya kuwa anawalipa mishahara karibu Tsh bilioni 4 kwa mwaka.
MO aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa
” Ninatangaza kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa bodi nitabaki kuwa mwekezaji na nitaelekeza nguvu zaidi kwenye miundombinu na soko la vijana,”