Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk. Hamisi Kigwangalla ametangaza kutoa kibano kwa Shirika la LGBT Voice Tanzania linalodaiwa kujishughulisha na kazi za kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja, kinyume cha sheria.

Kupitia barua yake, Kigwangalla amemtaka Mkurugenzi wa Shirika hilo, James Wandela Ouma kufika ofisini kwa Naibu Waziri huyo mapema leo asubuhi akiwa na nyaraka halisi zinazoonesha usajili, majina ya wanachama pamoja na Katiba ya Tanzania.

“Aidha, wanatakiwa kuwasilisha taarifa zinazoonesha miradi inayotekelezwa na shirika hilo, walengwa wa miradi ya shirika, wafadhili wa miradi na wadau wanaoshirikiana katika utekelezaji,” imeeleza barua ya Kigwangalla.

Aliongeza kuwa kushindwa kutekeleza agizo hilo kutapelekea kuchukuliwa hatua kali za kisheria dhidi ya shirika hilo.

Alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatoa taarifa kwa Mamlaka zinazosimamia sheria pale wanapoona watu au vikundi vya watu wanajihusisha na shughuli zinazohusiana na mapenzi ya jinsia moja.

 

Kala Pina akosoa wimbo mpya wa Chid Benz, adai amewaangusha mashabiki
Kubenea afunguka baada ya Serikali kulifungia gazeti la Mseto