Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa sanamu iliyochongwa kuashiria kuwa ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambayo hivi karibuni lilizua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii litafanyiwa marekebisho.

Katika uzinduzi wa hifadhi ya Burigi iliyoko Wilaya Chato mkoani Geita Waziri Kigwangala, alimkabidhi Rais Magufuli mfano wa sanamu la Mwalimu Nyerere, huku watu mbalimbali wakidai sanamu hiyo haikuwa na uhalisia na Mwalimu Nyerere.

“Baba wa Taifa alitoa tamko la kwanza la Uhifadhi nchini, ambalo ndiyo dira yetu, tuache dhihaka kwa sababu hakuna aliyefanya kazi ile kwa kusudi hilo, tumesema linashughulikiwa tunaomba mtuamini, mtupe muda turekebishe.”amesema Kigwangalla

Aidha, amesema kuwa kilichomfurahisha ni kuwa kizazi cha vijana wa kisasa, bado kinamkumbuka vizuri Baba wa Taifa, kinamuenzi na kumheshimu sana, ndiyo maana wanaikumbuka taswira yake, ambapo amesema watatumia vizuri zaidi wataalamu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kabla ya kuitumia.

Hivi karibuni kwenye uzinduzi wa hifadhi ya Burigi Waziri Kigwangalla alimkabidhi tuzo maalum ambayo hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilishinda kwa ni hifadhi bora barani Afrika.

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha sita
LIVE KAGERA: Rais Magufuli akizungumza na wananchi mkoani Kagera