Waziri wa maliasili na utalii ambaye pia ni mbunge wa Tabora Nzega vijijini, Khamis Kigwangalla ameibua mjadala mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter mara baada ya kuzungumzia juu ya ajira na ujasiliamali akionesha kuwashangaa vijana wanaolilia ajira baada ya kujiajiri wenyewe na kuwa wajasiliamali.

Moja ya jambo lililozua gumzo ni pale alipoandika kuwa alipohitimu digrii alianzisha kampuni iliyokuwa ikimuingizia Bilioni 10, ambapo wafuasi wake wengi kwenye mtandao huo wamehoji kwanini aliacha biashara na kuingia kwenye siasa.

”Mimi nilianza kujiajiri nikiwa nimemaliza form 6 kwa kuuza mchele mashineni, kufundisha Tuition, n,k. Nilipokuja chuo nilifungua saluni za kunyoa nywele ‘Barber shop’, Salons, biashara ya taxi na n.k na nilipohitimu digrii nilianzisha kampuni pamoja na mwenzangu na kukuza mzunguko mpaka zaidi ya bilioni 10” ameandika Kingwalla.

Ameongezea kuwa duniani kote hakuna serikali inayoweza kutoa ajira kwa wahitimu wote wa vyuo vikuu na hii ni kutokana na upungufu wa ofisi.

Hivyo ametoa wito kwa watu kuacha kusubiri mazingira wezeshi au kusubiri ajira kwani siku nazo hazigandi hivyo ametaka watu kuwa wajasiliamali ili waweze kujitengenezea kipato.

”Mjasiliamali ni mtu anayetengeneza fursa ya kilimo cha umwagiliaji jangwani na siyo mbugani” amemalizia Kigwangalla.

 

Bernd Leno kutambulishwa kaskazini mwa London
Mahakama yamkalia kooni daktari aliyeiba moyo wa marehemu