Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamis Kigwangalla amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa wanyamapori wa hifadhi ya Serengeti, kwa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Ameyasema hayo wakati akizungumza ndani ya Hifadhi ya Serengeti, ambapo amefanya ziara ya kushtukiza Dkt. Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyama Pori, Prof. Alexander Songorwa mara moja.

“Juzi usiku zilizunguka taarifa kwamba Dkt. Kigwangalla yupo na msafara wa gari mbili binafsi njiani kwenda Loliondo na kwamba atalala Hotel ya Acacia iliyopo Karatu. Leo msafara wangu umekuwa ukifuatiliwa na watu wasiojulikana ambapo kila hatua aliyofikia ilikuwa ikiripotiwa kwenye mtandao,”amesema Kigwangalla

Hata hivyo, Prof. Songorwa amekuwa akihusishwa na kashfa ya kushiriki kugawa vitalu vya uwindaji kinyume cha sheria pamoja na tuhuma nyingine.

Beki wa zamani wa Stoke City afariki dunia
Wenger awatupia lawama waamuzi Uingereza