Polisi Kata ya Dimani Wilaya Kibiti ambaye pia ni Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Samwel Kihongole amewaasa Wanafunzi kuwa na jitihada binafsi za kujifunza, ili kupata ufaulu wenye tija.

Kihongole alitoa wito huo wakati akiongea na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zimbwini na kuwashauri Wanafunzi hao kusoma kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuacha utoro na kuepuka vishawishi vinavyoweza kukatiza ndoto zao.

Aidha, amewashauri pia Wanafunzi hao kama wanawadogo zao kuwakumbushe Wazazi au Walezi kuwapeleka katika vituo vya kujifunzia elimu ya awali, ikiwa ni maandalizi ya kuwapeleka shule za msingi wakishafikia umri sahihi.

Katika maongezi hayo, Wanafunzi hao walipewa namba za mawasiliano ili wapeleke kwa wazazi kwa ajili ya kuripoti matukio ya uhalifu na wahalifu huku wakilipongeza Jeshi la Polisi kwa kupatiwa uelewa wa viashiria vya uhalifu na kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia.

Wakaguzi wa Polisi watakiwa kutumikia viapo vyao
Utamaduni kuiombea Nchi uendelezwe - Dkt. Mwinyi