Mwanafunzi mmoja wa Shule kongwe iliyopo jimbo la Maryland nchini Marekani, amefungua shauri Mahakamani, akitaka kubadili jina lake na la ukoo ili baadaye asije kuwa mlevi.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18, amesema amefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa watu saba wanaotumia jina hilo ndani ya ukoo wake ni walevi kupindukia.

Usikilizwaji wa kesi katika Mahakama ya Rufaa Maryland. Picha ya AP.

Mbele ya Mawakili na Hakimu wa Mahama Rufaa Maryland nchini Marekani, kijana huyo amesema ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili, kwani jina hilo (linahifadhiwa), ambalo ni urithi kutoka kwa babu yake lina historia mbaya.

Hata hivyo, wakati kijana akifikia uamuzi huo kwa hati ya kiapo kupitia kwa Mawakili wa Taasisi ya kulinda haki za watoto ya Maryland, Baba yake mzazi ambaye pia anatumia jina hilohilo, amemtaka atafute ukoo wa kuhamia mara baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu.

Vijana tumieni fusra za Kilimo kujiajiri - Dkt. Tulia
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 5, 2023