Hali ya simanzi imewakumba wananchi wa Mtaa wa kinyambwa Road uliopo kata ya Kikuyu jijini Dodoma, baada ya Kijana mmoja Yohana Luhanga (30), kumkata kwa mapanga na kumuua Bibi mmoja ambaye anadaiwa alimnyima mboga za majani na kukata makuti ya Mnazi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Martin Otieno amesema ni kweli mauaji yametokea katika eneo hilo na kusema Bibi huyo anakadiriwa kuwa na miaka 95-100 na aliuawa kwa kupigwa panga maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Amesema, “chanzo cha tukio ni huyu Kijana Yohana kuomba kukata makuti na Bibi yule alimuambia hawezi kuifanya kazi ile peke yake bali akatafute vijana wenzie ili wamsaidie, na ndipo Yohana akachukizwa na kitendo hicho na kuanza kumkata na mapanga maeneo mbalimbali ya mwili wake.”

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest amesema katika uchunguzi wa awali, unaonesha sababu za kupelekea umauti wa Bibi huyo ni kupoteza damu kwa wingi na majeruhi ambaye ni kijana amelazwa wodini na anaendelea vizuri.

Maafande Ligi Kuu kuweka kambi Shinyanga, Zanzibar
Christian Zigah asaini kandarasi mpya Dodoma