Kijana mmoja nchini Morocco amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela au faini ya Dola 4,000 baada ya kumtukana Mfalme wa nchi hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa Yuotube.
Mohamed Sekkaki alikamatwa mapema mwezi huu baada ya kukosoa hutuba ya Mfalme Mohamed na kumuita nyani wa Morocco.
Duru za habari kutoka nchini humo zimeeleza kuwa Sekkaki amepanga kukata rufaa dhidi ya shitaka hilo.
Kesi hiyo ilipelekea waandishi wa habari pamoja na mwanaharakati wa haki za binadamu, Omar Radi kukamatwa mwezi April kwa kumtusi Jaji wa shtaka hilo.
Kwamujibu wa wakili wa Sekkaki, mteja wake amerudishwa rumande mpaka januari 2, mwakani.
Mfalme Mohammed vi, alitoa baadhi ya madaraka yake kwa Serikali iliyochaguliwa baada ya maandamano wa mwaka 2011 lakini wachambuzi wanaona mfalme bado anapaswa kutoa neno juu ya masuala muhimu zaidi nchini humo.