Wakati uandikishaji wa daftari la kudumu la kupiga kura ukiendelea, kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Ikuzi Kicheko (Mzalendo halisi), ameshangaza watu kwa kuvaa mavazi yaliyokuwa yanavaliwa na watumwa enzi za ukoloni huku akiwa amebeba bango linaohamasisha watu kwenda kujiandikisha.

Kicheko amesema lengo la kufanya hivyo ni kuwepo kwa muamko hafifu wa wananchi kwenye kwenye zoezi la kujiandikisha kuchagua viongozi wa serikali za mitaa hali iliyopelekea serikali kuongeza muda wa zoezi hilo.

“Unajua nilivaa yale mavazi ni kuashiria kuwa kama Watanzania, tunawajibu wa kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura ili kuwapata viongozi tunaowahitaji na kuachana viongozi ambao wanafanana na Mfalme Sultani, ambao walikuwa wanaangalia zaidi maslahi yao binafsi na kuwa mfano wa kiongozi mbaya” amesema Kicheko.

Katika hatua nyingine Kicheko amesema kuwa lengo sio kuwaambia watu kuna utumwa, ila ni kuwaambia nenda ukajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura, epuka kuwa mtumwa nenda kajiandikishe ili upate kiongozi unayemtaka.

Octoba 17, 2019 ndio mwisho wa kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura ambapo serikali iliongeza siku tatu za kujiandikisha, ili kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika november 24, 2019

 

 

Magufuli amuwashia moto Mbarawa
TMA yatangaza mvua kubwa siku mbili