Mawaziri Sita, watatu kutoka Tanzania na Watatu upande wa Zambia wameingia makubaliano ya kuongeza na kuimarisha ulinzi wa Bomba la Mafuta la TAZAMA, kutoka jijini Dar es Salaam hadi Ndola.
Mara baada ya makubaliano hayo, Mawaziri hao walizungumza na Waandishi wa Habari na kusema wamefikia hatua hiyo baada ya bomba hilo kubadilishiwa matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hadi kusafirisha mafuta safi ya Dizeli ili kudhibiti matukio ya uhalifu wa wizi wa mafuta kwenye bomba hilo.
Mkutano huo uliandaliwa na Wizara ya Nishati, chini ya Waziri wake January Makamba na kuhudhuriwa na Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Innocent Bashungwa.
Kwa upande wa Zambia alikuwepo Waziri wa Nishati wa Zambia, Mhandisi Peter Kapala, Waziri wa Ulinzi wa Zambia, Ambrose Lufuma na Waziri wa Mambo ya Ndani, Jacob Mwiimbu.