Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limesema kuwa halijawaita wala kufungia wimbo wa Parapanda ulioimbwa na wasanii wa kundi la Rostam, Roma Mkatoliki na Stamina na kusema kuwa labda wameamua kujifungia wenyewe kwa lengo la kutafuta ‘kiki’.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Katibu wa Baraza la Sanaa, Godfrey Mngereza, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa hawajaufungia wimbo huo na haujapitishwa mikononi mwao hadi sasa kwa ajili ya kuhaririwa
“Labda kama wameamua kujifungia wenyewe ili kuufanya wimbo wao ujulikane na watu, lakini sisi hata hatujauona na kuupitia kama taratibu zetu zinavyotaka na mnajua tukifungia wimbo huwa tunatangaza sasa labda Roma awaonyeshe wapi tumesema hivyo,” amesema Mngereza..
Aidha, kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Roma kupitia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno ya kuilaumu Basata kwamba inaua vipaji na ubunifu wa wasanii na kuhoji wimbo wao huo una tatizo gani.
Wasanii hao, Agosti 2 waliachia wimbo huo Parapanda, unaoelezea masuala mbalimbali yanayoendelea nchini yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
-
Rais wa China ajibu ombi la JPM
- Dkt. Kalemani apiga marufuku TANESCO, REA kuagiza vifaa nje ya nchi
- Nafasi za ajira kutoka makampuni 8 Tanzania
Hata hivyo, katibu huyo amekiri kuwa juzi wasanii hao wawili kufika katika ofisi za Basata kwa ajili ya kushiriki jukwaa la wasanii ambalo hufanyika kila siku ya Jumatatu katika ukumbi wao uliopo Ilala Gereji huku mada kuu kwa siku hiyo ilikuwa kuhusu kanuni mpya za sanaa zilizoanza kutumika Julai mwaka huu.