Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi amesema, Serikali ilitangaza matumizi ya kanuni mpya ya mafao (Kikokotoo) ya pensheni kuanzia Julai 1, 2022 kupitia Gazeti la Serikali Namba 357 toleo la Mei 20, 2022.

Ameyasema hayo wakati akijibu msawali ya wabunge waliosimama kuuliza maswali ya nyongeza, wakilalamika kuhusu kikokotoo hicho, ambapo Swali la msingi limeulizwa na Mbunge wa Moshi Mjini (CCM), Priscus Tarimo, aliyehoji nini mpango wa Serikali kuhusu malalamiko ya wastaafu juu ya kikokotoo kinachotumika katika upigaji wa mahesabu ili waweze kulipya mafao yao.

Swali hilo pia, lilifuatana na lile la Mbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni, aliyehoji kuwa ni lini Serikali itapeleka Bungeni sheria inayohusiana na kikokotoo hicho ili wakakifute kwa madai watumishi hawakitaki.

Katambi amesema kanuni hiyo iliandaliwa kwa kuzingatia haja ya kuboresha na kuwianisha mafao ya wanachama na kuifanya mifuko ya pensheni kuwa endelevu.

“Mpango wa Serikali ni kuendelea kuwaelimisha wananchi hususani waajiri na wanachama wa mifuko ya pensheni wakiwemo wastaafu kuhusu faida ya kanuni mpya ya mafao ya pensheni,” amesema Katambi.

Aidha amesema, Serikali kupitia mifuko hiyo, na kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), imejipanga na inaendelea kutoa elimu ya kanuni hiyo ambapo hadi kufikia Juni 30, 2023, mifuko iliweza kutoa elimu kwa jumla ya waajiri 5,580 (PSSSF 362 na NSSF 5,218) kati ya waajiri 6,200 waliopangwa kufikiwa kipindi hicho.

Aidha Naibu Waziri Katambi amesema wanachama 131,497 (PSSSF 35,133 na NSSF 96,364) walifikiwa na mafunzo hayo.

Sofyan Amrabat ashinikiza kuondoka
Ya Bandari Bunge lilimaliza kazi yake - Spika Tulia