Bibi anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya 60 ameiomba serikali kupitia wizara ya ardhi imsaidie kurejesha ardhi yake yenye ukubwa wa ekari 120 ambayo amedai kuporwa na mfanyabiashara mmoja aliefahamika kwa majina ya Lukule Mponzi.

Kata ya Ihanga kijiji cha Mgala ndiko alikokuwa akiishi, Agness Lugala kikongwe kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, anasema baada ya kuugua alilazimika kwenda Dodoma kupatiwa matibabu kwa muda mrefu kidogo na alipokuwa huko alipewa taarifa za eneo lake kuvamiwa.

“Mimi hatukuonana na Mponzi aseme mimi nimuuzie niliona amekamata ardhi yangu, naomba serikali inisaidie nirudishiwe ardhi yangu,kwenye eneo langu kuna kaburi na vitindi vya ulanzi”amesema bibi Lugala

Mbilisila Mhenga ni mtoto wa bibi huyo ambaye amesema “Pale walikuwa wakiishi wazee wangu na huyu Mponzi ni wa Lupembe ilikuwaje aingie kuchukua ile ardhi, mimi Mponzi simjui, tunaomba serikali itusaidie mzee abakiwe na ardhi yake”

Mzee Mponzi anaelalamikiwa amekana kwamba hakuna anachokijua na wala hana kesi na mama huyo pamoja na kusema kuwa hajapoka ardhi hiyo.

“Mimi sijanyang’anya ardhi na sina kabisa ugomvi, tafadhari nikwambie  mimi hapa nilipo bado miaka miwili kuwa na miaka themanini sio mtoto wa kuchezea niongee nae taka taka wanini wakati amenipeleka mahakamani, siwezi kuongea kuongea nayeye wakati amenifikisha mahakamani” alisema Mzee Lukule

Serikali ya kijiji imetolea ufafanuzi kupitia mwenyekiti wake mpya aliechaguliwa hivi karibuni, huku diwani wa kata ya Ihanga ndugu Alfred Msingwa akisema kwamba uongozi uliopita ulikiuka taratibu za ugawaji wa maeneo baada ya kugawa maeneo hayo yaliyokuwa yameachwa kwa muda bila kuendelezwa.

“Hii migogoro ilisababishwa na viongozi wa awamu iliyopita kwasabu watu walikuwa wanagawa ardhi kiholela na hasa serikali za vijiji lakini tumejaribu kuwahamasisha watu kwasasa wanajua umuhimu wa ardhi” alisema Alfred Msigwa.

Kaimu mkuu wa idara ya ardhi bwana Lusubilo Mwakafuje, amesema umiliki wa ardhi usio kuwa na mashaka hususani vijijini, mtu akikaa kwenye ardhi kwa muda wa zaidi ya mika kumi na mbili bila kubugudhiwa inahesabika ni mmiliki wa halali wa hiyo ardhi  kwa mujibu wa sheria ya ukomo wa sheria ya ardhi.

Bunge laridhia Trump kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, urais wake ‘rehani’
Wanasheria waaswa kutowasahau waishio vijijini