Klabu ya Young Africans imetoa orodha ya wachezaji watakaosafiri kesho Jumapili (Agosti 15) kuelekea Morocco kwa ajili ya kambi ya majuma mawili, kujiandaa na msimu mpya 2021/22.

Kikosi cha wachezaji 27 kimeanikwa hadharani na kuondoa sintofahamu iliyokua inawatesa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo ambao walikua wanahitaji kufahamu nani na nani atakuwa safarini.

Ni dhahir kikosi kilichotangazwa ndicho kitakuwa na jukumu la kuipambania Young Africans msimu ujao wa Ligi Kuu na Michuano ya kimataifa msimu ujao 2021/22.

Walinda Lango ni Djigui Diarra, Erick Johora na Ramadhani Kabwili.

Mabeki wa pembeni ni Djuma Shabani, Kibwana Shomari, David Brayson, Yassin Mustapha na Adeyum Saleh.

Mabeki wa kati nu Yannick Bangala, Abdallah Shaibu Ninja, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.

Viungo Wakabaji na washambuliaji ni Khalid Aucho, Zawadi Mauya, Mukoko Tomombe, Saido Ntibazonkiza, Feisal Salum ‘Feitoto’ na Balama Mapinduzi.

Viungo wa pembeni ni Jesus Moloko, Farid Mussa, Deus Kaseke, Dickson Ambundo ba Ditram Nchimbi.

Washambuliaji ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Yaccouba Sogne na Yusuph Athumani.

Majaliwa atoa maagizo kwa wasimamimizi wa vituo vya umeme nchini
Benchi la ufundi Taifa Stars laboreshwa