Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia Rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amemteua Profesa William-Andey Anangisye kuwa makamu mkuu wa chuo hicho.

Prof. Anangisye ameteuliwa katika nafasi hiyo kuitumikia kwa miaka mitano, ambapo Makamu mkuu huyo mpya wa chuo anachukua nafasi ya Profesa Rwekaza S. Mkandala ambaye anamaliza muda wake.

Aidha, Dkt. Kikwete amefanya uteuzi huo baada ya kushauriana na bodi ya chuo kwenye kikao kilichofanyika Novemba 30 na baadae kumjulisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Hata hivyo, kabla ya uteuzi wa Prof. Anangisye alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Elimu Dar es salaam (DUCE). Pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambaye aliteuliwa na Rais Mgaufuli.

 

Mpina amwamuru mwekezaji kuondoka
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 6, 2017