Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa wakati wa maneno matupu kuhusu kuwashirikisha wasichana katika masomo ya Sayansi na Teknolojia umekwisha.
Ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa 30 wa Umoja wa Afrika (AU) Mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo Kikwete ni mwanachama wa tume ya kimataifa kuhusu ufadhili wa elimu duniani.
Amesema kuwa takwimu kuhusu masomo ya Sayansi Barani Afrika bado zinaonyesha kuwa watoto wa kike wako nyuma ukilinganisha na wakiume.
Aidha, ameongeza kuwa ni wajibu kwa Serikali za nchi wanachama kufadhili programu za elimu maarufu kama ‘STEM’ na kuweka vipaumbele kwa watoto wa kike sambamba na mapendekezo ya tume ya Umoja huo.
“Ni wakati wa nchi wanachama wa AU kuchukua hatua madhubuti ambazo zitalipatia suala hili msingi imara wa kisheria na kitaasisi katika kuwasaidia watoto wa kike kwenye suala hili.”amesema Kikwete
-
Museven amsifu Trump
-
Wanafunzi wachomana visu kwa kubishania dini
-
Rais Kagame kuteta na Trump kuhusu Afrika
Hata hivyo, mkutano huo umehudhuriwa na mabalozi wa nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ambao wanawakilisha nchi zao kwenye makao makuu mjini Addis Ababa.