Rais Jakaya Kikwete ameweka wazi msimamo wake kuhusu kauli zinazotolewa na mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli akiikosoa vikali serikali yake na kuhubiri kuhusu mabadiliko atakayoyafanya endapo atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alisema kuwa haoni tatizo lolote wala hashangai kusikia mgombea huyo akiikosoa serikali yake kwa kuwa Tanzania inahitaji muelekeo mpya.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo mjini Washington, Marekani aliopokuwa akiongea na wafanyakazi wa Taasisi ya NDI yenye uhusiano na Chama Cha Republican, IFES na United States Institute of Peace (USIP).

Alisema kuwa alifuatwa na watu mbalimbali wakimueleza kuhusu kauli za Dk. Magufuli kwenye majukwaa ya kampeni lakini aliwaambia kuwa jambo hilo ni sahihi na jema.

Niliwaambia nchi yetu inahitaji mawazo mapya na mwelekeo mpya ulio tofauti na uongozi wangu. Niliwaambia tusiporuhusu jambo hilo kufanyika, nchi yetu itabakia pale pale ambapo nimeifikisha mimi,” alisema Rais Kikwete.

“Haya yatakuwa ni makosa makubwa sana kwa sababu nchi yetu lazima isonge mbele kwa mawazo mapya na staili mpya ya uongozi,” aliongeza.

Chris Brown Kuzuiwa Kuingia Australia Kisa Rihanna
Ukawa Wadai Utafiti Twaweza Ni ‘Kichekesho’ Wataja Tafiti Zinazompa Ushindi Lowassa