Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimeunda kamati ya waangalizi wa uchaguzi kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 nchini Kenya.
Kamati hiyo iliyozinduliwa yenye wajumbe 52, itaongozwa na aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Timu hiyo maalum, inatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kuhusu uchaguzi huo Agosti 11, 2022.
Kikwete, amekuwa akiongoza misheni za waangalizi wa uchaguzi barani Afrika, ambapo ujumbe wake wa hivi karibuni ulikuwa nchini Zambia, ambako aliongoza timu inayowakilisha Jumuiya ya Madola.
Mwaka2019, Rais huyo mstaafu alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kundi la Waangalizi wa Jumuiya ya Madola, wakati wa uchaguzi mkuu wa nchini Nigeria.
Shughuli kuu ya waangalizi wa uchaguzi, husaidia kujenga imani ya umma na kujenga uaminifu katika mchakato mzima wa uchaguzi.