Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Dk. Jakaya Kikwete ambaye ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Tanzania inahitaji rais mkali baada ya kuondoka yeye ambaye wanamchukulia kama mpole.

Dk. Kikwete aliyasema hayo jana wakati akimnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli katika katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Morogoro na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Aliwataka wananchi hao kumchagua Dk. Magufuli kwa kuwa anakubalika hata ndani ya chama chake kwa kuwa alipata zaidi ya kura 2000 kati ya kura 2400 zilizopigwa na halmashari kuu ya chama hicho kumpitisha kuwa mgombea urais.

Alisema endapo wananchi watamchagua Dk. Magufuli watakuwa wameiweka nchi katika mikono salama.

“Nikiiacha nchi mikononi mwa Magufuli, nitalala usingizi kwa kuwa najua nchi itakuwa katika mikono salama,” alisema Dk. Kikwete.

Dk. Kikwete alimnadi mgombea huyo kwa wakazi wa Morogoro na kumuelezea kama mchapakazi na muadilifu anaefaa kuwa rais wa Tanzania.

Gwajima Kumrudishia Dk Slaa Kesho
Magufuli Kuwanyang’anya Mashamba Wawekezaji