Rais Jakaya Kikwete ameeleza nia yake ya kumtaja mmiliki wa kampuni ya Richmond iliyohusika katika ufisadi wa tenda ya ufuaji wa umeme wa dharura mwaka 2007/08.

Rais Kikwete aliweka wazi nia yake hiyo jana katika viwanja vya Lake Tanganyika mkoani Kigoma alipokuwa anawaaga wananchi wa mkoa huo, ambapo alionesha kumshangaa mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mmiliki wa Richmond.

Alisema anashangaa kuona Tundu Lissu anamtaka amtaje mwenye Richmond wakati anazunguka naye mikoani.

“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Rais Kikwete.

Picha Ya Lowassa Yasababisha Kifo
Lushoto Kutopiga Kura Ya Ubunge