Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amesema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassani ukiibibu kwenye maendeleo inakupigia amesema hayo wakati wa mwendelezo wa ziara yake kwenye Jimbo lake la Chalinze akisikiliza kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akieleza mipango mikubwa ya maendeleo inayokuja kwa Wananchi kwenye maeneo yao kutoka ngazi ya Halmashauri mpaka Taifa.

Ridhiwani ameutaka Uongozi wa Vijiji, Kata na Halmashauri kupata tathmini ya taarifa ya kero zilizopo na upungufu kwenye maeneo mbalimbali ya utoaji huduma kwa Wananchi ili inapoombwa Bajeti ya maendeleo lisisahaulike jambo na fedha ipatikane ya kutosha huku akiwataka Watumishi kuhakikisha kero zote zilizotolewa na Wananchi kwenye mikutano yake ziwe zinatekelezwa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Posi ambaye alieleza ofisi yake kuanzia Jumatatu itatuma Wataalamu kufanya tathmini ya changamoto ili haraka fedha ipelekwe kwa ajili ya kumaliza changamoto hasa ya uchakavu wa nyumba za Walimu, madarasa, umaliziaji wa Kituo cha Polisi Kwa- Mduma na zingine zikichukuliwa kwa ajili ya kusukumwa zaidi juu kwa ajili ya utekelezaji kama lile suala la changamoto ya mawasiliano.

Suala la maji pia linakwenda kuwa historia ambapo katika eneo la Kwa- Msanja panajengwa Bwawa kubwa la Maji ambalo litahudumia wakazi wa Chalinze.

RC Makalla: Magorofa 20 kujengwa kwaajili ya madarasa Dar
Mtahiniwa ajifungua na kuendelea na mtihani wodini